×

Global FC Usiwachezee!

KAMA hujui maana ya pasi au kampakampa tena kawaulize TSJ FC. Hawaji kurudia kuomba mechi na Global FC. Juzi Ijumaa walikumbana na kipigo cha mabao 2-0.

 

Katika mbungi hilo lililopigwa kwenye Uwanja wa St. Mary’s Tabata Jijini Dar es Salaam, timu hiyo ya Chuo cha Habari cha Times ilikumbana na wakati mgumu baada ya kushindwa kuwamudu Global ambao kipindi cha pili Kocha Amran Kaima ‘Zahera’ aliamua kuchezesha wachezaji wengi wa kikosi cha pili baada ya kuwaonea huruma wapinzani.

Baada ya mechi hiyo kumalizika mratibu wa wanafunzi wa TSJ, Conrad Massawe alikiri walizidiwa kila idara ila wanakwenda kusuka kikosi upya.

MARCO MZUMBE, Dar

SHEREHE ZA MWAKA MPYA WA KIISLAM, MUFTI AONGOZA