The House of Favourite Newspapers

‘Speakers Conference’ Yatikisa Dar – Pichaz

HATIMAYE ule mkutano wa kihistoria na wa aina yake uliopewa jina la Speakers Conference umefanyika leo Jumamosi katika Ukumbi wa Mikutano wa Kilimanjaro uliopo Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na mamia ya watu kutoka kada mbalimbali.

Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Global Group, Eric Shigongo akizungumza wakati wa hafla hiyo.

 

Speakers Conference (Season 2) umeanza  majira ya saa 2:30 asubuhi na utamalizika jioni ya leo majira ya saa 10:00 jioni huku watoa mada mbalimbali wakizungumza na kutoa mbinu mbalimbali hasa kwa vijana  ili kujitegemea na kuanzisha biashara za ndoto zao ili kuyafikia mafanikio yao.

Mkutano huo umewakutanisha  wahamasishaji wa masuala ya maendeleo na mafanikio, washauri, walimu wa ujasiriamali, watangazaji na waandaaji wa vipindi vya redio na televisheni, wafanyabiashara, wakufunzi, wajasiriamali na wahamasishaji chipukizi na watu wengine wa kawaida.

Lengo kubwa la mkutano huo ulioandaliwa na Taasisi ya Road to Success ni kuwajengea uwezo vijana wa kuzitambua fursa kutoka katika maeneo wanayoishi na kuzifanya kuwa biashara ili ziwaingizie vipato na kujikwamua kimaisha,  hivyo kuondokana na umaskini ama utegemezi wa ajira kutoka serikalini ama mashirika mbalimbali.

Miongoni mwa watu waliohudhuria katika mkutano huo, ni Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Global Group, Eric Shigongo ambaye pia ni mhamasishaji na mwalimu wa ujasiriamali,  Sophia Mbeyela, Chris Mauki, Anthony Luvanda, Harris Kapiga na wengine kibao.

Paul Mashauri akizungumza jambo wakati wa semina hiyo.

 

Akizungumza wakati akitoa somo, Shigongo alianza kuwaeleze historia ya maisha yake alipoanza masuala ya uhamasishaji mwaka 1999 hadi hivi sasa ambapo kikubwa amesema mtazamo wa watanzania hivi sasa wanauelewa juu ya masuala ya uhamasishaji na kwamba hasa tunakoeleka ni sehemu nzuri na wananchi waendelee kuunga juhudi za wahamasishaji ili kufikia malengo yanayohitajika. Pia amewataka vijana kufanya mambo manne ili wafikie mafanikio ambayo ni kupunguza matumizi yao hasa yasiyo ya lazima, kufungua macho yao na kuzitafuta fursa mahali zilipo, kuhakikisha wanawaridhisha wateja wao na mwisho ni kulinda himaya zao (biashara).

Picha ya pamoja ya baadhi ya wahamasishaji wa masuala ya ujasliamari.

 

Mkutano huo ulidhaminiwa na Global Publishers Ltd, EFM, MC Rhevan Online, Happiness Massage Clinic, FAPI, FABI Events, Megafin, Singo na SUS.

 

Comments are closed.