×

Bi Samia Atoa Heshima za Mwisho kwa Mwili wa Nelson Mabeyo

Makamu wa Rais, Samia Suluhu akimfariji Mkuu wa Majeshi Nchini Jenerali Venance Mabeyo kutokana na kufiwa na Mtoto wake aliyepatata ajali ya ndege wakati Makamu wa Rais alipofika nyumbani kwa Jenerali Mabeyo Msasani Jijini Dar es salaam leo Septemba 25,2019.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameungana na mamia ya waombolezaji na viongozi mbalimbali katika kuaga mwili wa mtoto Mkuu wa Majeshi nchini, Jenerali Venance Mabeyo aitwaye Nelson Mabeyo ambaye alifariki kwa ajali ya ndege juzi Jumanne, Septemba 23, 2019, Soronera katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

Samia Suluhu Hassan akimfariji mke wa  Jenerali Venance Mabeyo kwa msiba wa mtoto wao. 

 

Marubani wenzake na marehemu Nelson Mabeyo wakiomboleza msiba huo.

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, George Simbachawene akiwafariji Jen. Mabeyo na mkewe.

 

Bi Samia akisaini katika kitabu cha maombolezo kwenye msiba wa mtoto wa CDF, Jenerali Mabeyo.
Bi Samia Suluhu Hassan akiaga mwili wa marehemu

 

 

Bi Samia Suluhu akiwasili msibani hapo na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.