
Katika kuhakikisha tunasogeza huduma zetu karibu zaidi na wananchi Kampuni inayooongoza kwa uzaliashaji wa mabati bora zaidi na vifaa vingine vya uezekaji ALAF Limited, imefungua Duka lake la maonesho katika eneo la KIGAMBONI mtaa wa FERI Mkabala na Kivuko cha feri wilaya ya Kigamboni Jijini Dar es salaam.

Duka hili la maoneshao litawanufaisha wanaanchi wa wilaya ya Kigamboni na maeneo ya jirani kwa
faida zifuatazo
-Kupata majibu ya haraka ya mahitaji yao
-Kujifunza kuhusu bidhaa mbalimbali za ALAF
-Kuweza kuweka oda za mahitaji yao ya mabati
-Kuweza kununua bidhaa mbalimbali za ALAF
– Kupata ushauri wa kitaalam kutoka kwa wataalamu wetu walio bobea kwenye fani ya upauaji.

TAAARIFA FUPI KUHUSU ALAF
ALAF ni sehemu ya kundi la makampuni ya SAFAL,linaongoza katika uzalishajia wa bidhaa za upauaji kwa kutumia malighafi za chuma katika bara la Afrika, likiwa na shughuli za uzalishaji katika mataifa 13 yaliyopo mashariki,kati na kusini mwa bara la Afrika.

Likiwa na uzoefu wa trakibani miaka 50 katika uzalishaji na biashara,ALAF LTD inaongoza katika uzalishaji wa bidhaa za upauaji wa dari kwa kutumia malighafi ya chuma nchini Tanzania. Ili kuimarisha bidhaa zake, bidhaa za Maalum zinauzwa na ALAF Limited kama bidhaa za kufunga za Fixtite, mabomba ya Steel na sehemu za Hollow na vifaa vingine vya thamani kwa kampuni ya ujenzi.
