×

Kisa Mkwanja! Wananchi Kijiji Kizima Wameuza Figo Zao

NI jambo la kustaajabisha! Kijiji cha Hokse nchini Nepal kimebatizwa jina jipya la ‘Kidney Village’ kufuatia takribani watu wote wanaoishi kwenye kijiji hicho kuwa wameuza figo zao.

Inadaiwa kuwa wakazi wa kijiji hicho hali zao za kiuchumi ni duni sana,  kitu kinachowasukuma kuingia katika biashara ya kuuza figo zao ili wapate fedha za kujikimu mahitaji yao.

Mkazi mmoja aliyetambulika kwa jina la Geeta mwenye miaka 37 alisema kuwa yeye na mume wake walisafiri mpaka kwenye hospitali moja huko nchini India ili kutolewa figo zao na kulipwa zaidi ya shilingi milioni tatu za Tanzania.

 

Aidha, familia hiyo ilitumia fedha hizo kununua kiwanja na kujenga nyumba, lakini kwa bahati mbaya nyumba hiyo iliangushwa na tetemeko la ardhi lililotokea kijijini hapo.

 

Kwa upande mwingine, madalali wanaofanya biashara hiyo ya figo wametajwa kuzunguka kila mara katika kijiji hicho na kuwashawishi wanakijiji hao kuuza figo zao.

ITAKULIZA! MSANII AVUNJIKA MGONGO KIMAAJABU, ASIMULIA KILICHOTOKEA!