PENINAH WANGECHI, raia wa Kenya aliyechomwa visu mara 17 na mume wake ameondoa kesi dhidi ya mumewe mahakamani na kusema kuwa amemsamehe.
Ameiambia mahakama haishi tena na mwanaume huyo, na hajashinikizwa kufanya uamuzi huo, hivyo mahakama ikaamuru kuachiliwa kwa Samuel Ndirangu.

Mwanamke huyo alichomwa visu hivyo kutokana na ugomvi katika ndoa yao ambapo mwanamme huyo alikimbia lakini baadaye akajisalimisha ambapo majirani walimkimbiza hospitali akiwa hajielewi.