SERIKALI imesema kuwa korosho zote moani Mtwara zimeuzwa na unasubiriwa msimu mpya wa zao hilo na kwamba, mamia ya miradi mbalimbali ya maji, barabara, afya na mingine imekamilika na kukabidhiwa kwa serikali.
“Mpaka kufikia Septemba tumekamilisha miradi ya maji 200 na zaidi kuna vituo 89 elfu na tumetumia Bilioni 339 kwenye hiyo miradi ya maji. Kwa upande wa mijini tumekamilisha mradi mikubwa 17, na zimeshatumika Bilioni 823, miradi mingine 35 inaendelea kutekelezwa hapa nchini tumebakiza Asilimia 15 tu kufikia asilimia 95 kwa Mjini.
Aidha, Dkt. Abbas amesema kuchelewa kwa malipo kwa baadhi ya wakulima wa korosho ni kutokana na makosa yaliyojitokeza katika taarifa za wakulima kwaajili ya malipo na kwamba serikali inaendelea na zoezi hilo kwa ambao bado hawajalipwa.
“Tumekuwa tukisema kwamba kama kuna wakati mtu unapaswa kujivunia kuidai serikali ni sasa sababu serikali inalipa madeni,.. serikali hii ni makini,.. Kuna tani zaidi ya 4,595.90 zitabanguliwa nchini na zaidi ya tani 211, 587 ambapo tani 107,187 zitapitia Bandari ya Dar, ” tani 104,400 kupitia Bandari ya Mtwara zitasafirishwa kwenda nje ya Tanzania.
“Hadi sasa zaidi ya tani 98,860 zimekwisha chukuliwa na kusafirishwa nje ya nchi kupitia Bandari za Mtwara na Dar sawa na asilimia 41 ya korosho zote na zoezi la kuondoa korosho iliyobaki kupelekwa kwa wanunuzi linatarajiwa kukamilika ifikapo Oktoba 21 mwaka huu. Lakini pia mazao mengine yamepata nguvu ya kuwekewa mifumo na hivyo wakulima kupata bei inayowanufaisha kwa kuwapa faida.
“Naomba kusisitiza tena, faida kubwa ya mchakato huu ni kwa wakulima kupata bei ya haki katika zao la korosho lakini funzo la korosho si tu limeweka mazingira mazuri zaidi katika misimu ijayo ambapo korosho itanunuliwa kwa mfumo madhubuti.
“Sisi kama Serikali tunaamini uamuzi wa kununua Korosho ulikuwa uamuzi sahihi na ulifanyika kwa wakati, na tulinunua kwa zaidi ya Bilioni 720 na wananchi walinunuliwa Korosho tani Laki 225.
“Niwahakikishie wakulima kwamba, mpaka kufikia Septemba 30, 2019 Korosho yote iliyonunuliwa na Serikali kutoka kwa Wakulima, iliuzwa kwa jumla ya wanunuzi 21 wa ndani na nje ya nchi. Niwaambie wakulma wa Korosho wasisikilize maneno ya watu ambayo ni maneno matupu hayana msaada kwao.
“Hivi juzi Nchi yetu imetambulika Kimataifa kupitia tuzo ambayo Waziri Mkuu wetu mstaafu,.. Mzee Dkt. Salim Ahmed Salim aliipata,.. na huyu ni Mwafrika wa kwanza kupata tuzo hii. Tanzania imeongoza katika nchi ambazo zina mikakati ya serikali inavyosaidia kuondoa umaskini miongoni mwa nchi za kusini mwa jangwa la Sahara. Umasikini umeshuka Kutoka 34.4% mpaka 26.8%” Dkt. Hassan Abbasi, Msemaji Mkuu wa serikali.
“Hatuwezi kurudi nyuma tumeamua kujenga mradi wa umeme wa mto Rufiji, na mpaka sasa tumeshatoa Trilioni 1, kati ya Trilioni 6 na mpaka ikimalizika miaka 3 tutakuwa tuko pazuri. Bilioni 10.24 zimelipa watoa huduma mbalimbali; zaidi ya Bilioni 2 kwa ajili ya wakandarasi na waandishi washauri.
“Kama kuna wakati ambao kuidai Serikali ni faida basi ni wakati huu, kwa sababu tunalipa madeni tumeendelea kulipa madeni na tunaendelea kuhakiki. Kati ya Julai na Septemba, 2019, jumla ya TZS Bilioni 85.72 zimetolewa ikiwemo Bilioni 50 za madai ya pensheni, bilioni 22 madai ya watumishi wa umma ikiwemo kiinua mgongo kwa wastaafu 3,019 na malimbikizo ya mishahara kwa watumishi 1,435,” amesema Dkt Abbas.
Akizungumzia sakata la wahujumu uchumi kusamehewa, Dkt Abbas amesema; “Wanaosema Serikali imevunja Katiba kuhusu suala la Wahujumu Uchumi, waelewe kuwa Katiba sio gazeti, wanatakiwa wasome vifungu vyote sio kusoma kifungu kimoja tu halafu unaenda mtandaoni.
“Kwenye hili la Watuhumiwa wa uhujumu uchumi, tumefanya utafiti ukitaka kutupinga ujipange kwanza, nitoe wito kwa wanasiasa hamuwezi kuwa wataalamu wa kila kitu yaani kila jambo unajua, Katiba, Afya, Elimu,” amesema Dkt Abbas.