×

Usiku wa Mabingwa… Nampepeche Amepepecha Bondia wa Moro

Bondia Issa Nampepeche (mstari mwekundu) na Ally Hamis wakirushiana makonde.

BONDIA wa ngumi za kulipwa nchini, Issa Nampepeche amefanikiwa kumchapa Ally Hamisi wa Morogoro kwa pointi katika pambano la usiku wa mabingwa lilofanyika jana usiku kwenye Ukumbi wa Club 361, Dar.

Bondia Maganga Kulwa (njano) akimpiga ngumi bondia Said Sudi.

Katika pambano hilo ambalo lilikuwa na upinzani mkali kwa mabondia hao lakini Nampepeche alionekana bora kutokana na kupiga ngumi nyingi za uhakika katika raundi zote sita kabla ya kutangazwa na mshindi na majaji.

Mabondia waliotwaa mikanda uya ubingwa ya kimataifa wakipongeza juu ya uringo.

Baada ya ushindi huo, Nampepeche alitamba kuwa suala la kushinda kwake lilikuwa lipo wazi kutokana na kufanya maandalizi makali kabla ya pambano hilo huku akimtaka mpinzani wake akubali kushindwa.

Kwa upande wa Ally Hamisi akiri kuwa yeye ni bondia mdogo kutokana na rekodi ya mambano yake huku akiamini kwamba hajapigwa kutokana na madai ya mpinzani wake kutumia muda mwingi kurusha makofi badala ya ngumi kwenye pambano hilo huku yakiwa chini ya udhamini wa  Gazeti  la Championi, +255 Global radio, Smart Gin, Glady Matata na Kiwango Security.

 Katika mapambano mengi, Maganga Kulwa amefanikiwa kutwang ‘vitasa’ vya maana mpinzani wake Said Sudi na kupelekea kushinda kwa pointi pambano ambalo lilikuwa la raundi nne.

 Bondia Abdallah Kingolwira kutoka Morogoro amefanikiwa kushinda kwa pointi katika  pambano la raundi nne dhidi  ya  Ahmed Pelembela wa Dar aliyechukua nafasi ya  Ibrahim Makubi aliyeshinda kupanda ulingoni kutokana na kuumwa meno yaliokuwa yamevimbisha mdomo.

Pia bondia Salum Omari amefanikiwa kumchapa kwa pointi William Joseph katika pambano la utangulizi ambalo lilikuwa la raundi nne.

Nampepeche akitangazwa mshindi kwa kumchapa kwa pointi Ally Hamisi

 

Na Ibrahim Mussa