×

Mrisho Mpoto Ajiunga Rasmi CCM

MSANII Mrisho Mpoto, leo Jumamosi, Oktoba 5, 2019 amejiunga rasmi na Chama Cha Mapinduzi (CCM), na kukabidhiwa kadi ya Chama hicho na Katibu Mkuu wake, Dkt. Bashiru Ally.

Tukio hilo limefanyika katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wa ndani na viongozi wa matawi wa chama hicho.

Katika mkutano huo, RC wa Dar, Paul Makonda, ametoa shilingi milioni 100, kwa ajili ya kuanzisha Mfuko maalum wa Viongozi wa Mashina ya CCM pamoja na Wajumbe wao.

Amesema amefikia hatua hiyo ili kuwawezesha kukopeshana wao kwa wao, na kuwawezesha kujikimu katika mahitaji yao.