The House of Favourite Newspapers

Kocha Ac Milan Afutwa Kazi Baada Ya Miezi Mitatu

Uongozi wa klabu ya AC Milan umemfuta kazi kocha wake, Marco Giampaolo akiwa na miezi mitatu na nusu tangu apewe mkataba wa kuifundisha timu hiyo.

 

Kocha huyo ameiongoza Milan kucheza jumla ya mechi saba msimu huu huku akishinda mitatu pekee.

 

Katika mechi hizo tatu za ushindi, Giampaolo ameiwezesha Milan kujikusanyia jumla ya alama tisa ikiwa kwenye nafasi ya 13 ya msimamo wa ligi.

 

Giampaolo alichukua mikoba ya aliyekuwa kiungo wa timu hiyo, Gennaro Gattuso mwenzi Juni mwaka huu ambaye aliondoka kufutia kushindwa kuiwezesha timu hiyo kupata nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya.

BALAA ! KAKA AMTIA MIMBA DADA’KE

Comments are closed.