×

Mkenya Aweka Rekodi ya Dunia Mbio za Marathon

MWANASHERIA wa Kenya, Eliud Kipchoge, amefanikiwa kumaliza mbio za masafa marefu (marathon) kwa kutumia muda wa chini ya saa mbili.

 

Akiwa amevalia jezi nyeupe na kusaidiwa na wanariadha saba wa kumuongezea kasi (pace makers), Kipchoge, ambaye ni bingwa wa dunia na Olimpiki wa marathon, alipita barabarani akiwa anashangiliwa.

 

Mbio hizo za Ineos Challenge zilifanyika Vienna, Austria, kuanzia Darajani na kumalizia kwenye bustani ya Prater ambapo aliweka rekodi ya dunia.

Kwa miaka mingi, muda wa kumaliza mbio za marathon umekuwa kuanzia saa mbili, lakini Kipchoge alipania kumaliza mbio hizo maalum kwa kutumia muda wa chini ya saa 1:59 na kuandika historia.

 

Huku mishale ya saa ikionyesha saa 1:59:40.2, bingwa huyo wa Olimpiki alivuka sehemu ya kumalizia na kuwa binadamu wa kwanza duniani kumaliza kilomita 42 chini ya saa mbili.