
Mkurugenzi wa kikundi cha Vicoba cha BUTA, Semeni Gama ameelezea jinsi kikundi hicho kilivyonufaishwa na benki ya ACB kwa kuongezewa mtaji wao na kuweza kununua magari, Bajaj na Pikipiki ambavyo vitatumika kuboresha kikundi hicho kwa kuzalisha pesa na kufikia malengo makubwa zaidi.

Semeni alisema hayo kwenye maadhimisho ya kila mwaka ya kikundi hicho yaliyofanyika Bunju, Dar jana Jumamosi.

Naye Meneja Benki ya ACB Tawi la Kijitonyama, Joachim Mowo alikipongeza kikundi hicho kwa uaminifu na nidhamu yao fedha iliyofanikisha kufikia malengo yao na kuwaomba wananchi wengine waachane na michezo ya upatu ya mitaani ambayo mara nyingi si salama na kuwataka kwenda kuhifadhi pesa zao ACB ambayo ina akaunti mbalimbali zikiwemo akaunti ya malengo ya LIP ambayo utaweza kujiwekea malengo ya kuchukua pesa zako kwa muda uliojipangia.
Akaunti inaweza kutimiza lengo lako la kununua kiwanja, nyumba, kulipa ada, mahari na mengineyo.
HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS /GPL