MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan. amefungua mkutano wa Mawaziri wa Sekta za Mazingira, Maliasili na Utalii wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) jijini Arusha.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki, amesema, mkutano huo utajadili mwenendo wa hali ya mazingira, mabadiliko ya hali ya hewa na hali ya utalii na misitu katika nchi za SADC.
Pia utajadili juu ya utekelezaji wa mikakati ya hifadhi na usimamizi wa mazingira na kupitia mikakati na miongozo juu ya masuala hayo katika kutekeleza majukumu ya kila nchi ndani ya SADC.
Aidha, Tanzania imekabidhiwa Uenyekiti wa Shirikisho la Mashauriano ya Kisheria la Asia na Afrika (Asian-African Legal Consultative Organization (AALCO) 58th Annual Session).
Mkutano huo umefunguliwa na mikutano ya Wataalamu wa Sekta ya Wanyamapori na mkutano wa Makatibu Wakuu wa Sekta za Mazingira, Maliasili na Utalii ulioanza leo Oktoba 21 hadi 24, katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam.