Ni SIMULIZI za wazee wafungwa wa maisha jela walioachiwa huru na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli Desemba 09, 2017, baada ya kukaa jela kwa miaka 43 wakitumikia kifungo cha maisha kutoka kifungo cha kuhukumiwa KUNYONGWA.
Baada ya Mzee Aloyce Mwalongo na Mzee Raphael Mlyuka kusimulia ya kwao, leo ni zamu ya Mzee Yohana Chengula kusimulia yaliyomkuta gerezani hata akakatwa mguu.