×

Wenye Ndoto za Ujasiriamali Wapata Mkombozi ‘NALA’ (Picha +Video)

ULE wakati wa watu kuilalamikia Serikali kuhusu suala la ugumu wa kupatikana kwa ajira nchini umefikia tamati sasa, kwa sababu njia ya wao kujiajiri wenyewe kwa urahisi zaidi imepatikana.

Kampuni inayoendesha Application ya kufanya miamala ya mitandao yote bila kutumia intaneti nchini NALA inayomilikiwa na Mjasiriamali, Benjamin Fernandez, Mtanzania aliyekataa kazi ya mshahara wa Tsh milioni 400 nchini Marekani.

Kampuni hiyo iliyojishindia tuzo mbalimbali kubwa ndani na nje ya Afrika imekuja ya shindano linaloitwa MAMA KASEMA ambalo litakuwa likikusanya mawazo ya kibiasha kutoka kwa watu mbalimbali na atakayekuwa na wazo bora zaidi ya wengine wote atakuwa mshindi na kujinyakulia kitita cha shilingi milioni 10 za Kitanzania.

Akizungumza wakati wa kutambulisha shindano hilo leo Jumamosi, oktoba 26, 2019, katika ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Makampuni ya  Global Group, Mwanzilishi wa NALA, Benjami Fernandez amesema kuwa shindano hilo lipo kwa ajili ya kufikia watu ambao wamekuwa na uhitaji wa msaada wa mitaji ya kuanzisha au kuendeleza biashara zao.

“Mimi kama Mtanzania, nasikia furaha na fahari kufanya kitu nchini kwangu ambacho kitakwenda kuwasaidia na watu wengine kama mimi nilivyosaidiwa baada ya kufeli huko Marekani na nikaweza kufikia malengo yangu.

“Hivyo basi, kupitia shindano hili naamini litafungua akili za watu wengi sana na tukaweza kulinyanyua Taifa letu kwa ujumla” alisema Benjamin.

Stori: Ammar Masimba