The House of Favourite Newspapers

Kisa JPM, Makonda Amtaka Idris Ajisalimishe Polisi Haraka

Mkuu wa Mkoa wa DSM, Paul Makonda amemtaka muigizaji maarufu wa vichekesho nchini, Idris Sultan kufika katika kituo chochote cha polisi ambapo atakuta ujumbe wake kutoka kwa RC huyo.

 

Makonda ametoa maagizo hayo kufuatia msanii huyo kuhariri picha ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli na kuweka sura yake, pia kuhariri picha yake na kuweka sura ya Rais Magufuli kisha kuichapisha kwenye mitandao ya kijamiii ikiwemo Instagram na Twitter.

Idris ameandika; “Kwa siku moja tukabadilishana kazi ili a-enjoy birthday yake kwa amani.

Kufutia tukio hilo, Makonda kupitia akaunti yake ya Instagram ameandika; Naona mipaka ya kazi yako huijuwi. Nenda sasa hivi kituo chochote Cha polic uwambie Makonda kaniambie nije utakuta ujumbe wako. @idrissultan”

Comments are closed.