×

Ndoa yamkera Lulu

STAA wa filamu za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ameibuka na kusema hakuna kitu kinachomkera kama watu kumuuliza kuhusu ndoa kwamba kwa nini hajaolewa mpaka sasa hivyo kutokana na hilo basi atajioa mwenyewe.  Akizungumza na Shusha Pumzi, Lulu amesema anachukia zaidi anapoulizwa swali hilo na ukizingatia wengi wanaomuuliza ni wanawake wenzake ambao nao hawajaolewa jambo ambalo linamshangaza.

“Yaani kila unapokutana na mtu anakuuliza ndoa bado jamani wakati yeye pia ni mwanamke na hajaolewa… hii inanikera sana kwa kweli. Wanaona kuolewa ni kitu kikubwa, niwaambie tu hata nisipoolewa nitajioa mwenyewe kwani shida iko wapi au nani anateseka?,” Alisema Lulu.

STORI: IMELDA MTEMA