The House of Favourite Newspapers

VIDEO: Aibu! Mke Amfumania Live Mumewe Na Denti Gesti/ Aangua Kilio Hadharani!

TANGU mwaka huu wa 2019 umeanza kuna matukio mengi yametokea, lakini hili limebeba aibu nzito zaidi, Gazeti la Ijumaa Wikienda lina ishu nzito.

Aibu hiyo imempata mume wa mtu aliyetajwa kwa jina la Filbert Sunamie, mkazi wa Kibada, Kigamboni jijini Dar, twende taratibu!

Iko hivi, Sunamie amejikuta akifedheheka baada ya kufumaniwa laivu na mkewe akiwa na denti kwenye chumba cha nyumba ya kulala wageni (gesti).

ENEO LA TUKIO

Tukio hilo lilijiri kwenye nyumba hiyo ya kulala wageni iliyopo Sinza-Madukani jijini Dar, majira ya saa 9:00 usiku wa kuamkia Ijumaa iliyoita.

Sunamie aliyetajwa kuwa mfanyabiashara mkubwa hapa nchini alinaswa na mkewe aliyejitambulisha kwa jina moja la Shani ambaye aliambatana na polisi waliokuwa na difenda.

Awali, wakiwa katika ratiba zao za kukamilisha majukumu yao ya kihabari, wanahabari wetu walipata taarifa za kuwepo kwa tukio hilo dakika chache kabla ya kufanyika.

 

WANAHABARI WETU WATINGA

Walichokifanya wanahabari wetu ni kujiweka sawa kisha kutinga eneo la tukio ndani ya dakika sifuri na kuungana na msafara wa polisi na mke aliyekuwa amepagawa kutokana na uhakika aliokuwa nao kwamba mumuwe huyo alikuwa chumbani na denti huyo.

 

KABLA YA FUMANIZI

Kutokana na kuwa na hamu ya kutaka kujua kilichokuwa kinaenda kujiri, wanahabari wetu ilibidi waulize kama mama huyo alikuwa na uhakika wa kuwepo kwa fumanizi hilo.

“Huyo binti ambaye mume wangu yupo naye chumbani ni mjukuu wangu. Ni mjukuu wa dada yangu kabisa hivyo na sisi ni mjukuu au mtoto wetu na ana umri wa miaka 19.

“Huyo binti yupo kidato cha nne na anaanza mitihani ya form four Jumatatu (leo).

 

“Kuhusu kujua kama mume wangu anatembea na mjukuu wetu, nimewafuatilia kwa muda mrefu na huyo binti alikuwa akiniambia kila kitu namna babu yake anavyomsumbua akimtaka kimapenzi.

“Huyu binti au tuseme mjukuu wangu anakaa Mwenge (Dar) maana ndiko anakosoma, lakini kule nyumbani (Kigamboni) huwa anakuja na kuondoka.

“Sasa leo nimeambiwa na watu wanaowajua kuwa mume wangu amemfuata huyo binti na anazurura naye kuanzia kule Msasani, tumepita huko kote hadi huku Sinza yupo na mjukuu wetu na sasa yupo naye chumbani gesti,” alisema mama huyo akiwa amepaniki ile mbaya.

 

Comments are closed.