The House of Favourite Newspapers

Wasiojulikana Wachoma Moto Ofisi ya Kata, Waacha Bangi – Video

MKUU wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mgwhira, amesema watu kadhaa wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoani humo kwa tuhuma za kuchoma moto ofisi ya Kata ya Soweto iliyopo Moshi, mkoani Kilimanjaro na kusababisha hasara ya kuungua kwa nyaraka pamoja na samani zilizokuwa ndani yake.

 

Awali tukio hilo liliripotiwa kufanywa na watu wasiojulikana, ambapo wamechoma moto ofisi ya Afisa Mtendaji wa Kata ya Soweto usiku wa kuamkia jana, Novemba 10, 2019, ambapo pia wamechoma nyaraka zilizokuwa ndani ya ofisi hizo.

 

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mgwhira, amesema kuwa moto huo ulianza majira ya saa 7 usiku ambapo majirani waliokuwa karibu na ofisi hiyo walianza kuuzima na baadaye kutoa taarifa polisi.

 

“Wale wahuni walivunja mlango na kuanza kuchoma moto kuanzia dirishani na  baada ya kutekeleza uhalifu huo waliacha ganda lenye njiti za kiberiti pamoja na misokoto ya bangi ndani yake,” amesema Mgwhira.

 

Aidha, Mgwhira amewataka wananchi kuwa watulivu wakati vyombo vya ulinzi na usalama vikiendelea na uchunguzi ambapo mpaka sasa baadhi ya watu wanashikiliwa wa mahojiano.

 

Comments are closed.