×

Bosi Msauzi wa Simba Aaanika Mikakati Yake

Senzo Mazingira wa pili kushoto akiteta jambo na Mhariri Mtendaji wa Global Publishers, Saleh Ally wa pili kulia.

 

Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba, Senzo Mazingisa ambaye ni raia wa Afrika Kusini leo, Alhamisi, Novemba 14, 2019, amefanya ziara ya kikazi katika ofisi za Kampuni ya Global Publisher inayochapisha magazeti bora nchini ya michezo ya Championi na Spoti Xtra.

Senzo Mazingisa akisaini kitabu cha wageni kwenye mapokezi ya ofisi za Global Group, nyuma yake ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Simba, Mulamu Ng’ambi.

 

Mbali ya magazeti hayo ya mengine ambayo siyo ya michezo ni Ijumaa, Ijumaa Wikienda, Risasi, Amani na Uwazi.

Senzo Mazingisa akizungumza jambo kwenye ofisi ya Saleh Ally, pembeni yake ni Mhariri wa Gazeti la Championi Jumatano, Philip Nkini wa kwanza kushoto na Mhariri wa Championi Jumatatu, Ezekiel Kitula.

Akizungumza katika ziara hiyo, Senzo amesema amepania kufanya makubwa ili kuipa Simba Sc mafanikio makubwa ya Kisoka Afrika na duniani.

Mulami Ng’ambi akisaini kitabu cha wageni kwenye ofisi za Global Group.

 

Katika ziara hiyo, Mazingisa akiwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Simba, Mulamu Ng’ambi walitembelea vitengo mbalimbali pamoja na kujionea shughuli za uzalishaji wa magazeti.

Senzo Mazingisa akisisitiza jambo.

 

Lakini pia alitembelea katika studio ya Global TV Online pamoja na studio za +255 Global Radio kutazama namna ambavyo habari zinachakatwa na vituo hivyo kisha kurushwa kwa jamii.

Senzo Mazingisa pamoja na waandishi wa gazeti la Championi na Spoti Xtra, Martha Mboma na Ibrahim Mussa wakimsikiliza Saleh Jembe, (hayupo pichani).

Kujua zaidi mambo mengi aliyozungumza Senzo, nunua Gazeti la Championi kesho Ijumaa, Novemba 15, 2019.

Senzo akizungumza na Saleh.

Senzo kwenye picha ya pamoja na Wahariri wa Championi, Kitula wa kwanza kushoto, Nkini wa pili kushoto, Waandishi Ibrahim Mussa na Martha Mboma.

Senzo na waandishi wa Championi na Spoti Xtra.

Senzo akielezwa jambo na kiongozi wa Global TV Online, Abdallah Ng’azi, mwenye miwani.

Senzo akiwa nje ya studio za +255 Global Radio.

Senzo ndani ya studio za +255 Global Radio.

Senzo akiwa na Mkurugenzi wa Global Group, Eric Shigongo, ofisini kwake.

Senzo na Ng’ambi akiagana na Saleh.

PICHA NA MUSA MATEJA | GPL