Miss Tanzania Ajitapa Kutwaa Taji la Miss World
Mrembo anayeshikilia taji la Miss Tanzania 2019-2020 Silyvia Sebastian amejitapa mbele ya Waziri wa Habari Sanaa Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe, kurudi nchini na taji la Miss World kwenye kinyang’anyiro kinachofanyika katika jiji la London chini Uingereza hivi wiki ijayo.
Silyvia alisema hayo jana wakati jioni akikabidhiwa bendera ya taifa na Waziri Mwakyembe katika Mgahawa wa The Grand uliopo Posta, Dar kwa ajili ya kwenda kuliwakilisha taifa.
Akizungumza na wanahabari amesema kwa kushirikiana na kampuni ya The Look waandaaji wa michuano hiyo wamejiandaa vya kutosha kufanya maajabu kwenye michuano ya mwaka huu yanayoshirikisha warembo 130 kutoka mataifa mbalimbali.
HABARI: NEEMA ADRIAN
PICHA: RICHARD BUKOS
Comments are closed.