×

Kitabu cha Utafiti wa Nishati ya Gesi, Madini Chazinduliwa

Balozi wa Norway hapa nchini, Elisabeth Jacobsen,  akizungumza na wadau kwenye uzinduzi wa kitabu hicho.

 

TAASISI ya Repoa na Wizara ya Nishati na Madini kwa kushirikiana na Ubalozi wa Norway jana wamezindua kitabu kinachohusu utafiti wa nishati hizo.

 

Wadau wakiwa makini kusikiliza kinachoendelea.

 

Kitabu hicho kinaelezea jinsi utafiti wa nishati hiyo ilivyofanyika hapa nchini huko Songosongo na Mnazi Bay na kujadili mambo mbalimbali ikiwemo faida ya nishati hizo itakavyoinua uchumi wa nchi.

Mgeni Rasmi, Sebastian Shana (kulia) akizindua kitabu hicho.

 

Akiongea katika uzinduzi huo uliofanyika Hyatt Regency Kilimanjaro Hotel, Dar, Kamishna Msaidizi wa Gesi wa Wizara ya Nishati, Sebastian Shana,  amesema gesi hiyo itasaidia maendeleo ya taifa ambapo mpaka sasa asilimia 54 ya gesi imeshaanza kutumiwa na shirika la umeme nchini (Tanesco).

Mgeni rasmi, Kamishna Msaidizi wa Gesi wa Wizara ya Nishati, Sebastian Shana, akionyesha kitabu hicho baada ya kukizindua.

 

Shana amesema pamoja kutumiwa na Tanesco,  itatumika pia kwa matumizi mengine ambapo tayari kuna magari 300 hapa nchini ambayo yameanza kutumia gesi hiyo.

Wadau wakionyesha kitabu hicho kwa furaha baada ya kuzinduliwa.

 

Katika uzinduzi huo wadau mbalimbali waliohudhuria waliupongeza utafiti uliofanywa kwenye kitabu hicho ambacho kitapatikana sehemu mbalimbali ikiwemo mtandaoni.

Shana akizungumza na wanahabari baada ya uzinduzi.

 

Mbunge wa Sengerema na Waziri Mstaafu wa Nishati na Madini, William Ngeleja,  akizungumza na wanahabari kama mdau.

HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS /GPL