TIMU ya Taifa Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars, na ile ya Zanzibar, Zanzibar Heroes, zimepangwa kundi moja, kuelekea katika Mashindano ya Afrika Mashariki na kati, (Cecafa).
Timu hizo zimepangwa katika Kundi C, sambamba na Kenya, Harambee Stars na timu ya Djibouti. Mashindano hayo yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi Desemba 7-19, mwaka huu, nchini Uganda, katika Mji wa Namboole.

Kundi A; Uganda, Burundi, Ethiopia, Eritrea. Kundi B; DR Congo, Sudan Kusini, Sudan, Somalia. Kundi C; Kenya, Tanzania, Djbouti, Zanzibar.
Kwa upande wa mashindano ya wasichana wa U17, timu zitakazoshiriki ni saba, zikipangwa katika makundi mawili, A na B, ambapo Tanzania imepangwa kundi B pamoja na timu za Burundi na Djibouti, huku kundi A kuna timu za Uganda, Ethiopia, Sudan Kusini na Eritrea. Mashindano hayo yataanza Desemba 9-18 katika mji wa Jinja, Uganda.
MARCO MZUMBE, Dar es Salaam