×

Azam FC Watoa Dozi Kwa Alliance, Waipiga 5-0 Nyamagana

 

Kikosi cha timu ya Azam kilichoanza dhidi ya Alliance kwenye Dimba la Nyamagana.

 

TIMU ya Azam FC leo Novemba 26, 2019 wanatoa dozi nene kwa Alliance kwenye Dimba la Nyamagana jijini Mwanza.

 

Mshambuliaji wao Obrey Chirwa ameonyesha mefunga ‘hat-trick’ kwenye ushindi wa bao 5-0,  alianza kuandika kitabu chake cha mabao dakika ya pili ya mchezo akiunganisha pasi safi kutoka kwa Shabani Chilunda ndani ya 18 ambayo ilimshinda mlinda mlango wa Alliance, Andrew Ntala.

 

Nyota huyo aliongeza bao la pili kabla ya mapumziko akipiga shuti kali nje ya 18 dakika ya 24 akimuacha Ntala asijue nini cha kufanya katikati ya milingoti mitatu.

Bao la tatu Chirwa amefunga dakika ya 67 ya mchezo ambalo lilitokana na kuachia mkwaju mzito nje ya 18 ambao ulimshinda kipa wa Alliance FC wakati mabao mawili yakifungwa na Chilunda.

Matokeo ya mechi nyingine

FT: Kagera Sugar 1-3 Mtibwa Sugar (Awesu Awesu 39’ : Juma Nyoso 65’ OG, Haruna Chanongo 78’, 90’+3)
.
FT: Mbeya City 1-2 Mwadui FC (Peter Mapunda 44’p : Merickiard Mazella 65’, Wallace Kiango 90’+3).
.
FT: JKT Tanzania 2-1 Ruvu Shooting (Jabir Aziz 15’, Adam Adam 17’ : Rajab Zahir 40’p).
.
FT: Alliance FC 0-5 Azam FC (Chirwa 4’, 25’, 68’, Chilunda 33’, 53’).
.
FT: Biashara United 1-0 Lipuli FC (Lenny Kisu 57’)