Kiduku Ammaliza Msauzi kwa TKO, Amtaka Dulla Mbabe (Picha +Video)
BONDIA Twaha Kiduku kutoka Morogoro, amemchakaza bondia kutoka Afrika Kusini, France Ramabolu, kwa TKO kwenye raundi ya tano ya mpambano wa utangulizi uliyokuwa wa raundi nane.
Hii ilikuwa ni kuelekea pambano kali ya raundi kumi kati ya Hassan Mwakinyo na Arnel Tinampay. Baada ya ‘game’ hiyo, Ramabolu ametoa malalamiko yake kwa mwamuzi na kusema mwenzake huyo alikuwa akicheza faulo nyingi lakini refa alizipotezea.
Twaha ambaye alikuwa akipiga ngumi za chapchap tangu mwanzo wa mchezo huo, alionekana kummudu Msauzi huyo tangu raundi ya kwanza mpaka raundi ya tano alipompelekea konde kali lililomwangusha na kumfanya Twaha aibuke mshindi.
Baada ya kumpiga Msauzi huyo, Twaha akamchokoza Dullah Mbabe na kumweleza kuwa anahitaji kupambana naye. Muda mfupi baadaye, Dullah alitokea palepale na kusema yeye ni bondia, na kazi yake ni kupigana, hivyo akamtaka Twaha atafute promota ambaye atamlipa vizuri na watakutana katika pambano.
PICHA NA RICHARD BUKOS | GPL