The House of Favourite Newspapers

Mimba ya Esma Yachoropoka Petit Akiwa Safarini

0

IKIWA ni miezi michache tangu arudiane na Baba watoto wake, Petit Man baada ya kuhitirafiana kwa zaidi ya mwaka mzima, dada wa msanii wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz aitwaye Esma Platnumz amekiri mimba yake kuharibika wiki chache zilizopita.

 

Akihosjiwa na Wasafi FM hivi karibuni, Esma ambaye alikuwa ameachana na Petiti huku kila mmoja akiishi kwenye mahusiano mengine, amesema tayari alikuwa ameshanasa ujauzito wa Petit ambapo walikuwa wakitegemea kupata mtoto mwingine, lakini kwa bahati mbaya mimba hiyo ikachoropoka.

 

“Nilikuwa na mimba siku ile Aunty Ezekiel ana birthday yake. Kweli Petit alisafiri aliporudi mimi nilikuwa hospitali kama Juma alivyosema, ndio hivo mimba yangu iliharibika ndio maana hukutuona pale kwa birthday ya Aunty.”

 

“Mimi na Petit tumerudiana imekuwa muda kidogo lakini wote tulikuwa katika mahusiano, yeye kwa yake mimi kwa yangu. Tuseme labda kitu kikubwa ni watoto ambao wameturudisha. Tahiya alikuwa ni wa kwanza yaani alikuwa anampenda Petit, Taraji naye pia hivo. Hata nikijaribu kuwaweka mbali lakini watoto utakuta wamempigia simu.

 

“Kuna wakati Petit anamchukua Tahiya na kumpeleka shopping, ukimuuliza hivi vitu kakununulia nani kuna wakati anaficha lakini kuna wakati anasema uncle Petit ndio kaniletea. Ilifika tu tukaona kila mtu awache mahusiano yake turuadiane,” alisema Esma.

 

Leave A Reply