The House of Favourite Newspapers

Tigana Kuzikwa Makaburi ya Msasani Dar

0

MWILI wa nyota wa zamani wa kimataifa wa Tanzania, Ally Yusuf ‘Tigana’ aliyefariki dunia jana mchana, unatarajiwa kuzikwa saa 10 jioni kwenye makaburi ya Msasani, jijini Dar es Salaam.

Tigana aliyezichezea klabu mbalimbali ndani na nje ya nchi zikiwamo Pan Africans, Yanga, Simba na Cadets ya Mauritius alikumbwa na mauti katika hospitali ya Amana baada ya kuugua ghafla alipoenda kumtembelea mkewe aliyelazwa hospitalini hapo kabla hali yake kubadilika akiwa nyumbani na kuwahishwa hapo akilalamika tumbo linamsyumbua kiasi cha akitapika na kuharisha.

Mmoja wa rafiki wa karibu wa familia ya marehemu na aliyewahi kucheza naye enzi za uhai wake, Mwanamtwa Kihwelu alisema, mazishi ya Tigana aliyezaliwan mwaka 1970 jijini Dar es Salaam utazikwa saa 10 jioni Msasani.

Leave A Reply