MKALI wa Hip Hop wa mamtoni, Robert Rihmeek Williams ‘Meek Mill’ amewajia juu wanaochochea mabifu ya wasanii na kuwaambia wao ndiyo wanachangia kuuharibu muziki na siyo kuukuza.
Meek aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kuwa anakerwa na kitendo cha baadhi ya watu kuingilia ugomvi ambao pengine wangewaachia wenyewe wahusika wangeumaliza na maisha yakaendelea kama kawaida.
Meek ameonesha kukerwa na kitendo hicho baada ya wale waliokuwa wakimtaja msanii wake anyefahamika kama Youngro777 kuwa na ugomvi na msanii mwenzake, Blueface Bleedm.
PHILADELPHIA, MAREKANI