Aliyewahi kuwa Balozi wa Tanzania nchini Urusi katika Serikali ya Awamu ya Nne, Balozi Jaka Mwambi amefariki jana Jumapili, Desemba 8, 2019.
Mtoto wake, Juvenile Mwambi amethibitishia kutokea kwa kifo hicho. Pia, marehemu aliwahi kuwa Mkuu wa Mikoa ya Tanga, Rukwa na Iringa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Bara.