
KUNA usemi usemao kuwa ukipenda boga penda na ua lake, ndivyo ilivyo kwa msanii wa filamu Bongo, Kajala Masanja ambaye anasema mwanaume yeyote anayehitaji kumuoa lazima ampende mwanaye, Paula kwanza.
Kajala ameiambia Over Ze Weekend kuwa hata mwanaume awe na mali kiasi gani lakini kama hana upendo na mtoto wake hawezi hata siku moja akampenda wala kuwa naye.
“Yaani ni heri nipite kwenye changamoto nyingi sana lakini ukweli ni kwamba kama mwanaume ananipenda tu mini na hampendi mtoto wangu basi hana nafasi kwangu,” alisema Kajala.
STORI: IMELDA MTEMA