MSANII wa muziki Bongo ambaye pia ni ‘video vixen’, Gift Stanford maarufu kama ‘Gigy Money’ amewataka wasanii wenzake wazae na kuacha dhana ya kuwa ukizaa utazeeka.
Akizungumza na Uwazi hivi karibu, Gigy alisema kuwa anawashangaa wasanii wengine ambao hawataki kuzaa kisa kuogopa kuukaribisha uzee;
“Nashangaa, eti msanii hataki kuzaa kisa anaogopa kuzeeka… mimi nimezaa, nimezeeka? siyo kwamba mwanamke akizaa anazeeka, hiyo inatokana na wewe mwenyewe unavyojitunza. Kwa wale waliojaaliwa kuzaa, wazae tu! Hawanioni mimi sasa hivi ninavyoinjoi na Mayra wangu? Haijalishi anatunzwa na baba au hatunzwi, napambana mwenyewe,” alisema Gigy.