×

King Limau na Marhaba Soap ni Habari Nyingine

      Promosheni ya nguvu ya sabuni za unga za King Limau na Marhaba Soap iliyofanyika kwenye maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam, imeweka rekodi ya aina yake kutokana na ubora wa sabuni hizo zinazozalishwa na Kampuni ya Azania Group of Companies!

Baada ya promosheni ya awali kuwagusa wananchi wa Manzese, Mabibo, Tandale na Sinza, safari hii ilikuwa ni zamu ya watu wa Karume, Tandika, Temeke na maeneo ya jirani!

Wakazi wa maeneo hayo, wamepata nafasi ya kujionea wenyewe jinsi sabuni hizo zinavyoongoza kwa kung’arisha nguo, kuwa na harufu nzuri na uwezo wa hali ya juu wa kuondoa madoa katika promosheni ya nguvu iliyofanyika mitaani.

 

Wananchi waliokuwa na bahati, wamegawiwa sabuni hizo bure kabisa, huku wakipata maelezo ya namna ya kuzitumia ili kupata matokeo bora kabisa katika usafi wa nguo.

“Hizi ni bidhaa mpya, wananchi wengi bado hawajapata bahati ya kuziona sabuni hizi za kisasa kwa hiyo tumezunguka kwenye maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar ili kuwafikia wananchi ambao tunaamini baada ya kusikia maelezo kutoka kwetu na kwenda kuzijaribu wenyewe, watakuwa mabalozi wazuri kwa watu wengine,” amesema Catherine Kahabi, kiongozi wa promosheni hiyo.

“Kwa kweli hizi sabuni ni nzuri sana! Mimi nimechana kidogo pakiti hapahapa na kunusa harufu yake, kiukweli imenivutia na naamini hii ndiyo itakuwa sabuni yangu mpya,” Tausi Kilomo, mama lishe anayefanya shughuli zake Tandika, alisema baada ya kupewa pakiti zake za bure za King Limau na Marhaba.

“Unajua hizi kazi zetu ni ngumu, tunachafuka sana na nguo kupata madoa sugu ni kitu cha kawaida kabisa, si unajua tena! Lakini kwa maelezo niliyoyasikia leo kwenye promosheni, naamini hizi sabuni zitanifaa sana, ngoja nikazijaribu, Juma Kigeu, mfanyabiashara wa Soko la Tandika alisema baada ya kufikiwa na timu ya promosheni za sabuni hizo.

Namna ya kujipatia sabuni hizo, ni rahisi sana! Nenda duka lolote lililo jirani na mahali ulipo, usiseme sabuni ya unga bali sema King Limau au Marhaba Soap na muuzaji atakupatia kwa bei nafuu kabisa! Kisha baada ya hapo, nenda kaijaribu mwenyewe na utaona matokeo yake!

 

Kwa mawasiliano zaidi, wapigie kwa namba 0710 111 112 au watumie barua pepe kwa anuani ya email: [email protected].

 

Leave a Comment