
Benki ya Akiba Commencial (ACB) jana iliungana na wanachama wa kikundi cha FATA Vicoba Endelevu kusherehekea kumaliza mwaka ambapo wanachama waliojiwekea faida kubwa katika kikundi hicho waliweza kujizolea zao katika hafla hiyo.
Katika hafla hiyo mgeni rasmi alikuwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaa mstaafu, Suleimani Kova ambapo Meneja Masoko wa ACB, Innocent Ishengoma aliiwakilisha benki hiyo iliyotajwa kuwapa elimu ya utunzaji wa fedha wanachama wa kundi hilo.

Baada ya kufanikisha malengo ya kikundi cha FATA, Ishengoma aliwatangazia wanachama hao akaunti mpya ya bendi hiyo iitwayo LIP ambayo inamuwezesha aliyefungua kutimiza malengo yake kwa kujiwekea muda wa kujichukulia fedha hizo kipindi alichojiwekea.
Ishengoma amesema akauti ya LIP inakuwezesha kujiwekea malengo mbalimbali kama vile kununua nyumba, kiwanja, gari, ada, au chochote ambacho una lengo nacho.

Ameongeza kwa kusema katika unaweza kujiwekea kiwango cha kuanzia 20,000/ kwa mwezi mpaka siku kufikia kipindi cha malengo yako.

Katika hafla hiyo Mwenyekiti wa kikundi hicho, Hanipha Tarimo aliishukuru benki ya ACB kwa jinsi wanavyowahifadhia fedha zao vizuri na kuwapa faida kubwa ambapo amewataka wananchi wengine kujiunga na benki hiyo.

Wanachama waliojiwekea faida kubwa kwenye hicho mama chenye vikundi vingine tisa walikabidhiwa vitita vya fedha ambavyo walivuna kama faida.