
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Upande wa mashtaka katika kesi ya mauaji inayomkabili Mfanyabiashara Hamis Said (38) umedai kuwa jalada bado lipo kwenye hatua ya mwisho ya uchapaji, ambapo kesi hiyo ilikuja mahakamani kwa ajili ya kutajwa, ambapo wakili Mwaikambo ameahirisha kesi hiyo hadi Desemba 30, mwaka huu.
Mshitakiwa anadaiwa Mei 15, 2019 katika eneo la Gezaulole Kigamboni, Dar es Salaam, alimuua mtu anayeitwa Naomi Marijani kisha kumchoma moto kwa kutumia magunia mawili ya mkaa ambapo alichukua majivu ya marehemu na kwenda kuyafukia shambani kwake mkuranga.