×

Washtakiwa kwa Kuweka Sumu Kwenye Chakula

 

MAMENEJA watatu wa shamba huko Baringo nchini Kenya, wamefikishwa mahakamani wakikabiliwa na shtaka la kuweka sumu kwenye chakula na kusababisha vifo vya watu wanne na wengine kuathirika.

 

Watu hao watatu ambao ni wasimamizi wa shamba walitambulika kwa majina ya Paul Kinyua,  Evans Oyugi na Nelson Letite ambao walikamatwa mwishoni mwa wiki na walifikishwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkazi,  Viennah Omboko,  Jumatatu.

 

Aidha, mwendesha mashtaka aliomba muda zaidi kuipitia ripoti ya taarifa za vifo (postmortem) ili aweze kuandaa mashitaka ambapo mahakama ilimpa siku 14 na kuamuru watuhumiwa hao wapelekwe rumande katika Kituo cha Polisi cha Marigat.

 

Kukamatwa kwa watu hao kunafuatia agizo lililotolewa na Gavana wa Baringo, Stanley Kiptis,  aliyehimiza uchunguzi kufanywa haraka baada wagonjwa 10 kulazwa katika hospitali ya Eldoret ambapo wanne kati yao walifariki.

 

Akifafanua zaidi kuhusu hali ya waathirika wa sumu hiyo katika hospitali ya kati huko Eldoret, Gavana Kiptis alisema wagonjwa watano wamehamishwa kutoka Hospitali ya Kabarnet na wawili kati yao bado wapo kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU) wakati watatu walikuwa wamehamishiwa Hodini wakiwa wanaendelea na dawa.

 

Sambamba na hilo, vipimo vya Daktari Parag Patil, vimeonyesha kuwa watu hao watano waliathiriwa na sumu ambayo ilileta madhara katika mifumo yao ya mishipa ya fahamu na ubongo.

 

Pia, taarifa zinaeleza kuwa jumla ya watu 17 ambao walikuwa wakifanya kazi katika shamba hilo walikimbizwa hospitalini siku ya Ijumaa ambapo mpaka sasa watu wanne wamethibishwa kufariki.

Leave a Comment