×

Yaliyojiri Mkutano Mkuu wa Chadema – Video

MKUTANO Mkuu Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)  unafanyika leo Jumatano, Desemba 18, 2019, katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, ambapo agenda kuu ikiwa ni uchaguzi wa mwenyekiti wa chama taifa na makamu mwenyekiti wake wawili, wa Tanzania Bara na Zanzibar.

Katika uchaguzi huo, wajumbe zaidi ya 1,000,  ambao watapiga kura kuwachagua Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chama hicho sasa na Cecil Mwambe, Mbunge wa Ndanda,  anayewania nafasi hiyo.

Wanaowania nafasi ya makamu mwenyekiti ni aliyekuwa mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu,  aliyepo nchini Ubelgiji.  Hata hivyo, Lissu ataomba kura hizo kwa njia ya mtandao wa Skype.

Katika nafasi hiyo Lissu anachuana na mbunge wa Viti Maalum, Sophia Mwakagenda.

Leave a Comment