×

LHRC Yaitaka Polisi Ieleze Alipo Magoti – Video

 

KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimeliomba jeshi la polisi kutaja kituo ambacho anashikiliwa mmoja ya wafanyakazi wake, Tito Magoti,  ambaye alikamatwa jana Ijumaa, Desemba 20, 2019, maeneo ya Mwenge jijini Dar es Salaam.

 

Mkurugenzi wa LHRC, Anna Henga,  amesema hayo leo Jumamosi, Desemba 21, 2019,  wakati akizungumza na wanahabari katika ofisi za kituo hicho zilizopo Kijitonyama jijini Dar es Salaam kuhusu tukio hilo.

 

Baada ya taarifa kusambaa jana kuwa Matoti  ametekwa, Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, ilisema inamshikilia  mfanyakazihuyo pamoja na watu wengine.

 

“Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam tunamshikilia Tito Magoti (26), Mkazi wa Ubungo-Kibo, Afisa Programu wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu ( LHRC ) pamoja na watu wengine watatu kwa uchunguzi na mahojiano kwa tuhuma za makosa ya jinai.

 

“Tito hakutekwa bali amekamatwa na polisi leo (jana) saa tano asubuhi maeneo ya Mwenge na yupo katika mikono salama, yeye na wenzake watatu wanaendelea kuhojiwa na watafikishwa mahakamani baada ya kukamilisha uchunguzi na mahojiano,” alisema  Mambosasa.

Leave a Comment