×

Video: Katibu Mkuu Mpya Chadema Azungumza Kwa Mara Ya Kwanza


Katibu Mkuu mpya wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Mnyika leo Desemba 22, 2019 ameongea na wanahabari na kuweka mikakati yake ya kwanza kwenye chama chake.

Akiongea na wanahabari Mnyika amesema haya: –

“Kazi yangu ya kwanza, kudai Tume Huru ya Uchaguzi kama ilivyoazimiwa na mkutano mkuu, Baraza Kuu na Kamati Kuu kwa kuzingatia kuwa chaguzi ndogo zilizosimamiwa Tume ya Uchaguzi (NEC) na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa zilizosimamiwa na Tamisemi zote hazikuwa huru wala za haki”

“Kazi yangu ya pili, kuanza mapema maandalizi ya wagombea wa udiwani, ubunge na urais, Kazi yangu ya tatu, ni kuratibu maandalizi ya ilani ya Chadema ya uchaguzi mkuu 2020”

“Lengo kuu la chama cha siasa ni kushiriki na kushinda uchaguzi Ili kuchukua dola na kutumia itikadi na sera zake kuongoza Serikali”

👇

kutazama mkutano wote.

Leave a Comment