×

Maua halewi sifa kwa sauti yake

 

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Maua Sama, amesema anajijua kuwa ana sauti nzuri na inapendwa kwa hiyo hawezi kujibweteka na kushindwa kufanya kazi nyingi na nzuri kisa kulewa sifa.

 

Akizungumza na Gazeti la Ijumaa Wikienda, Maua alisema kuwa unakuta mtu mwingine anaimba vizuri lakini kwa vile amesifiwa na watu wengi analewa sifa ambapo kwa upande wake hapendi iwe hivyo licha ya kwamba anajua ana sauti nzuri na inayopendwa na wengi ila haimleweshi na kuanza kuvurunda.

 

“Najitambua kuwa mimi ni mwanamuziki mzuri, nina sauti nzuri lakini sitaki kulewa sifa hata kidogo kwani nikifanya hivyo nitajikuta navurunda na kuharibu kabisa muziki wangu,” amesema Maua.

Stori: Imelda Mtema, Ijumaa Wikienda | DAR

Leave a Comment