×

Madam Ritha: BSS Imebadilisha Maisha ya Vijana Wengi

Madam Ritha ndani ya studio za Global Radio.

 

 

MDAU wa tasnia ya sanaa nchini, Rita Paulsen almaarufu kama Madam Ritha ambaye ni mwanzilishi wa shindano la kuibua vipaji vya sanaa ya muziki ‘Bongo Star Search (BSS)’ amefunguka na kusema kuwa shindano hilo limefanikiwa kubadilisha maisha ya vijana wengi waliowahi kushiriki au kupita katika shindano hilo.

 

Hii inakuja baada ya kuwa na tetesi mitaani kuwa wasanii ambao wanatoka katika shindano hilo huwa hawavumi wala kufanikiwa kwenye tasnia ya muziki licha ya kufanya vizuri katika shindano hilo.

 

Madama Ritha akisalimiana na Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho ofisini kwake.

 

Kupitia mahojiano na kipindi cha Bongo255 cha +255 Global Radio, Madam Ritha amekanusha uvumi huo  na kusema; “Kila mtu atafanikiwa katika njia zake mwenyewe, sio kila mtu atakuwa kama Diamond au Vanessa Mdee. Hakuna mtu aliyewahi kupita BSS akawa na maisha ya kawaida wengi wamebadilika sana.

 

 

“Watu wanapenda kuongea vitu visivyo vya kweli ingekuwa vizuri wafanye utafiti kwa wasanii wote waliotoka BSS wako na maisha gani ndio waje na majibu ila wasanii wote waliopita BSS wamebadilika maisha yao kwa asilimia kubwa,” amesema Madam Ritha.

 

Mhariri wa Gazeti la Championi Jumatatu, Ezekiel Kitula akimfafanulia jambo Madam Ritha.

 

Aidha, aliongeza kwa kuwataja wasanii hao ambao ni Walter Chilambo, Haji Ramadhan, Kayumba, Frida Amani na wengine wengi ambao wamefanikiwa kutoka sehemu moja na kufika nyingine.

“Wote walifika BSS hakuna aliyewahi kuwafahamu kabla, lakini BSS ikawapa nafasi ya kufahamika na leo wapo kwenye jamii wanafanya vizuri zaidi,” alisema Madam Ritha.

Leave a Comment