×

Amber Rutty Kuhusu Kufumaniwa na Enock Bella

 

VIDEO vixen na msanii, Amber Rutty, amefunguka kusema aliwahi kufumaniwa na mume wake Davil, akiwasiliana na msanii Enock Bella ambaye alikuwa anamtaka kimapenzi.

 

 

Rutty amesema wakati anafanya kazi ya “video vixen” alitakwa kimapenzi na wasanii wengi ambapo mmoja wao alikuwa ni Enock Bella.

 

 

“Wasanii wengi walinitaka ila siwezi kuwataja nisije nikawapa kiki bure, maana kuna wasanii wanatafuta kiki na wanakufuata makusudi ili uwazungumzie kwenye mahojiano ila wapo wengi hata hamsini wanafika ila ipo siku nikicharuka nitawaanika katika mtandao wa Instagram” amesema.

 

 

Ameongeza: “Ninachowaambia wajipange sana, nina mume wangu nampenda hatari kwa hiyo wanajisumbua, sasa hivi nawastiri kwa pua maana kwa mdomo nitawaumbua, ninayemkumbuka mmoja wapo ni Enock Bella mpaka Davil alitufumania kwenye meseji na wengine wengi”.

 

 

Leave a Comment