MAPENZI ya awamu ya pili yananoga eeh? Hii imedhihirishwa na staa wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel ambaye ametoa kali kwa kusema kama unataka kushushiwa vita ya pili ya dunia, basi mwanamke yeyote ajitokeze amchukue mpenzi wake, Moses Iyobo.

Akizungumza na Risasi Jumamosi, Aunt amesema ameshaona watu wanaanza kumnyemelea tena baba watoto wake hivyo amewapa tahadhari mapema sana kuwa wasiitafute vita isiyokuwa ya lazima.
“Jamani kama mtu anaitafuta vita ya pili ya dunia basi ajaribu kumfuatafuata baba Cookie maana tulivyokuwa hatupo pamoja walikuwa hawamfuati sasa amerudi ndiyo wanataka kuleta shobo, nadhani hawanijui vizuri,” alichimba mkwara Aunt ambaye ni takriban miezi miwili sasa tangu arudiane na baba mtoto wake huyo.