×

Dkt. Mpango Aanika Hali ya Uchumi, Utekelezaji wa Bajeti – Video

WAZIRI wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango amesema ongezeko la deni limetokana na mambo mawili,  kwanza ni riba ya mikopo ambayo mikataba yake iliingiwa zamani, pili ni mikopo mipya yenye masharti nafuu na ile ya kibiashara, kwa ajili ya kugharamia miradi ya maendeleo.

 

Amesema hayo leo Jumanne, Desemba 31, 2019, wakati akitoa tathimini ya utekelezaji wa bajeti ya serikali ya mwaka 2019/20 kwa kipindi cha miezi sita ya mwazo jijini Dodoma na kusema deni la taifa bado ni himilivu kulingana na viwango vya kimataifa ikiwamo kulingana na pato la taifa.

 

“Novemba 25 hadi Desemba 30, 2019 mashirika 137 yamewasilisha michango kwa kuchangia kiasi cha Shilingi bilioni 19.6, hadi sasa bado mashirika na makampuni 50 ambayo hayajachangia. Septemba 2019 mapato ya kodi yalivunja rekodi ya makusanyo tangu tupate uhuru baada ya kukusanya trilioni 1.7, natoa pongezi nyingi sana kwa kamishina na atumishi wote wa TRA.

 

 

“Thamani ya Shilingi ya Tanzania imeendelea kuwa tulivu, tangu Julai mpaka Novemba 2019, Dola moja ilibadilishwa kwa wastani wa Shilingi za Tanzania 2,291, ikilinganishwa na shilingi 2,276 kwa mwaka 2018,” amesema.

 

 

Leave a Comment