×

Polisi 29 Wahukumiwa Kifo


MAHAKAMA Kuu nchini Sudan imewahukumu kifo polisi 29 kwa kosa la kumtesa na kumuua Mwalimu Ahmad al-Khair (36) waliyemkamata wakati wa maandamano ya kupinga utawala wa Rais Omar al-Bashir.

Inadaiwa kuwa baada ya polisi kumkamata Al-Khair walimpiga na kumtesa hadi kufa. Hakimu amesema kuwa hukumu za kifo ni sehemu ya kutoa funzo kwa watu juu ya uvunjaji wa sheria.

 

Mwanasheria wa upande wa watetezi anasema kuwa atakata rufaa. Hii ni moja ya kuhumu za mwanzo kabisa kutolewa mara baada ya machafuko ya kuleta utawala wa demokrasia nchini Sudan, yaliyosababisha watu 170 kuuawa.

Leave a Comment