
MWIZI arejesha sanduku lenye majivu ya marehemu baada ya kuliiba sanduku hilo ndani ya gari la familia ya marehemu walipokuwa wakielekea kuyazika.
Majivu hayo yalikuwa ni ya mwili wa kijana aliyefahamika kama Dennis Bebnarz ambaye alifariki dunia katika ajali ya gari miezi mitano iliyopita.
Familia ya Dennis Bebnarz imesema walipanga kumwaga mabaki ya Dennis katika sehemu yenye utulivu na nzuri baada ya kifo chake na walichagua Cyprus lakini sanduku lenye majivu ya mwili ya Dennis liliibiwa nyuma ya gari lao, wakati wenyewe walipoenda kula chakula katika mgahawa.
Mama yake Dennis, Kinga Bebnarza amesema mwizi huyo alimpigia simu akiwa analia na kuomba msamaha kwa kitendo alichokifanya na akawaelekeza sehemu ambayo watalikuta sanduku hilo.
Siku ya Jumapili ya Dec 29 wanafamilia hao walisafiri kuelekea nchini Poland baada ya kukosa matumaini ya kuyazika majivu ya mtoto wao.