
BAADA ya kufanya vibaya kwenye michezo miwili ya Ligi Kuu England iliyopita leo kocha wa Arsenal, Mikel Arteta, atakuwa tena uwanjani kupambana na Man United.
Huu utakuwa mchezo wa pili kwa Arteta nyumbani baada ya wikiendi iliyopita kulala kwa mabao 2-1 dhidi ya Chelsea kwenye Dimba la Emirates baada ya kuongoza kwa bao 1-0 zaidi ya dakika 80.
Arteta aliichukua timu hiyo kutoka kwa Friedie Ljungberg, ambaye alikuwa anaishikilia kwa muda lakini bado mpaka leo hajapata ushindi kwenye michezo miwili aliyoiongoza baada ya kupoteza mmoja na sare mmoja.
Leo atakuwa uwanjani kupambana na Man United ambayo kwa siku za karibuni imeonekana kuamka na kuanza kufanya vizuri kwenye ligi ikiwa mechi yake ya mwisho iliwachapa Burnley mabao 2-0.

United ambayo inaongozwa na mshambuliaji wake kinda Marcus Rashford ipo nafasi ya tano kwenye msimamo ikiwa na pointi 31, leo itataka kupata ushindi ili kuisogelea Chelsea ambayo ipo nafasi ya nne na pointi 35.
Vijana wa Arsenal kama watapoteza mchezo huu watakuwa kwenye wakati mgumu kwa kuwa kwa sasa wapo katika nafasi ya 12 wakiwa na pointi 24, zikiwa ni pointi sita mbele ya timu ambazo zinaweza kushuka daraja mwishoni mwa msimu na pointi 11 dhidi ya timu iliyopo nafasi ya nne kwenye msimamo.

Timu zote mbili zina mawazo ya kumaliza kwenye nne bora tu msimu huu kwa kuwa hakuna hata moja ambayo
Alikuwa inaweza kutwaa ubingwa. Michezo mingine mikubwa ya leo, Manchester City watacheza na Everton, Southampton watakipiga na Tottenham Hotspur huku Newcastle wakivaana na Leicester City.