
UCHUNGUZI wa Gazeti la IJUMAA unathibitisha, pasi na shaka kuwa, wanaume walio wengi hasa barani Afrika, wanapagawa na kuvutiwa na mwanamke mwenye shepu ya kuvunja chaga.
Kwa lugha rahisi wanajua kuwamezea mate wanawake wenye kalio kubwa (mzigo) ambao nao inasemekana wanajiamini kutokana na kupendelewa na Mungu wao.

Kwa mfano, wanawake mastaa wenye kalio kubwa kama Kim Kardashian, Jeniffer Lopez ‘JLO’, Nicki Minaj, Vera Sidika, Sanchi na wengine ndiyo wamekuwa wakitumika kama kivutio kwenye mitandao ya kijamii ili kuwavutia wanaume kununua bidhaa mbalimbali.
Kuthibitisha hilo, katika kipindi cha sikukuu za hivi karibuni, zilisambaa video za mrembo mwenye figa la hatari, aliyejaaliwa kalio la baab’kubwa na kuwa gumzo kuwa huenda ndiye mwanamke namba moja mwenye shepu matata zaidi duniani.
Gazeti la IJUMAA lilijipa kazi ya kutafuta mrembo huyo ni nani hasa kiasi cha kusababisha baadhi ya wanaume kukosa utulivu ambapo kwa mujibu wa vyanzo vya kuaminika, mrembo huyo anaitwa Jacqueline almaarufu Jaye Love, ni Mmarekani mweusi mwenye asili ya Afrika.
Jaye Love ni kweli ana picha nyingi mtandaoni zinazomuonesha na shepu hilo linalowapagawisha wanaume kila anakoalikwa kwani ni mrembo maarufu mtandaoni (sociolite), ni MC, DJ na mtu anayelipwa kwa kutokelezea kwenye shughuli mbalimbali (appearance).

Mrembo huyu wiki iliyopita alisababisha taharuki kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kotoka nchini Ghana baada ya kutua nchini humo kwa shughuli maalum ya kusimamia sherehe ya ‘madoni’ fulani wa nchini humo huku kila mwanaume akimtazama na kumrekodi video.
Baadhi ya wanaume walikwenda mbali zaidi na kusema kuwa hawakuamini kama mzigo huo ni wake na kwamba walidhani unadondoka.
Mrembo huyu ana umbo la kipekee na Mungu amemjaalia kalio kubwa, kiasi cha kutikisa ulimwengu wa wanaume.
Akiwa kwenye uwanja huo wa ndege, kila alipopiga hatua, wanaume walibaki wakimeza mate na wengine kusisimkwa kiasi cha kujikuta wakiangua vicheko na miguno.
Wapo waliodhani labda amefungia mzigo wa magendo kwenye sehemu hiyo kabla ya kuona ni kali lake mwenyewe.

Wengine walijikuta wakimuonea wivu mpenzi wake na wengine wakisema kuwa jamaa yake anahitaji pongezi kwa kumiliki mzigo huo.
“Hii ni hatari, naapa, sijawahi kuona mwanamke aliyejaliwa kiasi hiki…” alisikika mwanaume mmoja kwenye video iliyosambaa ikimuonesha mrembo huyo akitembea na kusababisha sintofahamu.
Mrembo huyo ana umaarufu mkubwa kwenye mitandao ya kijamii hasa Instagram kutokana na umbo lake hilo huku akiwapiga kikumbo warembo matata wa Bongo wenye mizigo kama Sanchi na Poshy Queen ambao wanaonekana ni cha mtoto mbele yake.
Makala: Mwandishi Wetu na mtandao