
WANAWAKE wengi wenye kisukari hupata tatizo la kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa. Hii inaweza kuwa ni moja ya dalili ya kisukari kwa wanawake. Hali hii mara nyingi huambatana na hasira za mara kwa mara. Mbali na kisukari, baadhi ya maradhi mengine yanayochangia tatizo la mwanamke kutokuwa na hamu ya kufanya tendo la ndoa ni saratani na matatizo ya akili.
Matumizi ya dawa huondoa hamu ya kufanya mapenzi kwa mwanamke mfano kutumia dawa za kukabiliana na msongo wa mawazo. Kati ya chanzo au sababu kuu ya aina ya pili ya kisukari ni mtindo wa maisha tunayoishi, matumizi ya pombe na uvutaji wa sigara pia huchangia kukosa hamu ya tendo la ndoa.
Pia, upasuaji uliofanyika katika maeneo ya maziwa au viungo vya uzazi huathiri ufanyaji kazi wa viungo hivyo na kumfanya mama kukosa hamu ya kufanya kitendo hicho. Kuna matatizo ya kisaikolojia ambayo pia yanaweza kumsababishia mwanamke kupata tatizo la kukosa hamu ya tendo la ndoa.
Matatizo ya msongo wa mawazo, kuhisi kutothaminiwa au kutokukubalika katika jamii, kuwa na historia mbaya katika uhusiano na historia ya kunyanyaswa kimwili au kijinsia kama kupigwa au kubakwa. Hali hiyo huathiri kiwango cha sukari kwa mwanamke hivyo husababisha kupanda.
Ni vema kujua dalili za mtu mwenye kisukari ambazo ni hizi zifuatazo:
- Kunywa maji mengi kuliko kawaida na kusikia kiu kila wakati.
- Kwenda haja ndogo mara kwa mara.
- Kuwa dhaifu, kukosa nguvu na kujisikia mchovu kila wakati.
- Kupungua uzito au kukonda licha ya kula vizuri.
- Kusikia njaa kila wakati na kula sana.
- Wanawake kuwashwa ukeni.
- Kutoona vizuri.
- Kwa wanaume; kupungua nguvu za kiume au hamu ya kujamiiana kwa wanawake.
- Ganzi, kuchomwachomwa au kutohisi unapoguswa sehemu za miguu, viganja na vidole.
- Miguu kuoza na hata kupata ganzi, kukauka kwa ngozi.
- Vidonda au majeraha sehemu yoyote ya mwili kutopona haraka.
- Kupata majipu mwilini.
- Kukojoa mkojo ambao mara baada ya dakika chache kama umekojoa chini ya udongo huzingirwa na sisimizi kwani wanafuata sukari.
Itaendelea wiki ijayo.