×

Mane Ashinda Tuzo Ya Mchezaji Bora wa Afrika 2019

Mshambuliaji wa Liverpool, Sadio Mane usiku wa kuamkia leo Januari 8, 2019 ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa Afrika 2019 baada ya kumpiku mchezaji mwenzake wa Liverpool, Mohamed Salah raia wa Misri na winga wa Manchester City na Algeria Riyad Mahrez.

Mane (27) aliisaidia Liverpool kutwaa ubingwa wa Ulaya mwaka 2018-2019 akifunga mabao 30 katika mechi za mashindano mbalimbali.

 

Pia alifunga mabao 15 msimu 2019-2020 na kuipa Liverpool pointi 13 katika msimamo wa Ligi Kuu England.

“Nina furaha kubwa kushinda tuzo hii. Mpira ni kazi yangu, naupenda. Napenda kuishukuru familia yangu, wachezaji wenzangu wa timu ya taifa, shirikisho na klabu ya Liverpool, leo ni siku yangu,”alisema Mane.

Wakati hafla ya utoaji tuzo ikifanyika Hurghada, Misri, Salah aliyetwaa tuzo hiyo miaka miwili iliyopita na Mahrez hawakutokea katika tukio hilo.

Leave a Comment