×

Netflix Kuifuta Filamu Inayomwonesha Yesu Kama ‘Shoga’

Mahakama yaamuru mtandao maarufu wa kuonyesha filamu, Netflix kufuta filamu inayoonyesha Yesu kama mtu anayeshiriki mapenzi ya jinsia moja.

 

Jaji mmoja huko Rio de Janeiro, Brazil ameamuru Netflix iache kuonyesha filamu “ya kufuru” ambayo inaonyesha Yesu kama mtu shoga.

 

Jaji Benedicto Abicair alitoa uamuzi huo katika kujibu ombi la shirika la Katoliki la Brazil ambalo lilisema kwamba filamu ya The First Temptation Of Christ ‘imewavunjia heshima mamilioni ya Wakatoliki.’

Uamuzi huo wa mahakama ni halali hadi mahakama nyingine itoe amri nyingine tofauti na hiyo. Filamu inaonyesha Yesu anarudi nyumbani siku ya kuzaliwa akiwa na miaka 30 na anaonyesha ni mtu wa kufanya mapenzi ya jinsia moja.

 

Baadhi ya Wakatoliki kupitia mitandao ya kijamii wameeleza kuchukizwa kwao na video hiyo huku wakiitaka Netflix kuiondoa haraka na kuwaomba radhi Wakristo wote duniani kwa kufanya ‘uchafu’ huo wa kudharirisha dini yao.

Leave a Comment